Alhamisi, 1 Septemba 2016

NGASA ALICHO-POST INSTAGRAM BAADA YA KUVUNJA MKATABA SOUTH AFRICA

Taarifa za Mrisho Ngasa kuvunja mkataba na klabu yake ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini zinazidi kuenea kwa kasi hususan kwenye mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa barua ya kuvunjwa mkataba huo iliyotolewa na Meneja Mkuu Rantsi Mokena inaonesha mkataba huo umevunjwa tangu August 25, 2016 na kwa maana hiyo Ngasa yupo huru kujiunga na timu yeyote watakayofikia makubaliano. Baada ya taarifa hizo huzidi kusambaa, Ngasa maarufun kwa jina la ‘anko’ ame-post picha inayoonesha akiwa katika timu mbalimbali ambayo imeambatana na ujumbe. “Thanks God am so happy now, dua zangu umekuwa ukiniitika kila ninapokuita. Picha ipi imekukumbusha mbali hapo ankali,” ni baadhi ya maneno yanayosomeka kwenye post ya Ngasa. “#I love my Tanzania#am free agent,” hivyo ndivyo Ngasa alivyomaliza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni