Jumapili, 18 Desemba 2016

Rekodi 6 zilizovunjwa baada ya Arsenal kufungwa na Man City. Ligi kuu England imeendelea Jumapili ya December 18 kwa mechi tatu kuchezwa kwenye viwanja tofauti. Game iliyopewa uzito wa juu na mashabiki wengi wa Bongo ni kati ya Manchester City vs Arsenal ambayo ilimalizika kwa Arsenal kupigwa 2-1. Arsenal walianza kupata goli mapema kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Theo Walcott dakika ya tano. Man City wakaja juu na kusawazisha kisha kuongeza goli jingine. Magoli ya City yamefungwa na Sane na Sterling yote yakikwamishwa nyavuni kipindi cha pili. Katika mchezo huo, rekodi sita zimevunjwa na kuwekwa nyingine mpya huku Man City wakipanda hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 36 nyuma ya Chelsea inayoongoza ligi ikiwa na point 43. Man City imeshinda kwa mara ya kwanza mchezo wa Premier League ambao walipoteza katika kipindi cha kwanza (tangu November 2012 vs Tottenham). Arsenal wamepoteza mechi tatu msimu huu ambazo walianza kuongoza zaidi ya walivyofanya katika msimu mzima wa 2015-2016 (walipoteza mechi mbili). Guardiola bado hajapoteza mchezo wowote wa nyumbani dhidi ya Wenger katika mashindano yote (W4 D1). Sane amekuwa mchezaji wa sita wa kijerumani kufunga goli ndani ya Premier League kwenye klabu ya Man City. Sterling amefunga goli kwa mara ya kwanza kwenye Premier League katika mechi tisa zilizopita tangu alipofunga dhidi ya Swansea City mwezi September. Cech amecheza mechi sita za Premier League bila clean sheet kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka. Matokeo ya mechi zingine za jana Bournemouth 1-3 Southampton Tottenham 2-1 Burnley

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni