Alhamisi, 1 Septemba 2016

Simba noti za kumwaga mezani MASTRAIKA Laudit Mavugo na Fredrick Blagnon ndiyo walioshikilia utajiri ndani ya Simba endapo watafanikiwa kufunga mabao kila mechi na kuipa ushindi timu hiyo ambapo hupewa kitita cha pesa kuanzia Sh 5 milioni kama motisha kwa wachezaji wote. Katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu, wadau wa Simba kutoka kundi la ‘Simba makao makuu’ walijichangisha Sh 10 milioni na kumkabidhi Meneja wao Mussa Mgosi lakini pesa hizo zilirudi katika mfuko wa wadau hao baada ya kutoka sare ya bila kufungana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni